Shetta Anusirika katika ajali ya Gari iliyotokea huko Babati Arusha,Baada ya gari kupinduka mara tatu

Hit maker wa Kerewa Shetta amesema anaendelea vizuri baada ya kupata ajali ya gari hapo jana maeneo ya Minjingu akielekea Babati kwa ajili ya kufanya show.



Akizungumza na moja ya wadau wetu wa arusha kupitia simu leo,Shetta,amesema kuwa mpaka sasa bado yupo Babati na ameshapata huduma ya kwanza ingawa bado ajisikii vizuri

Tazama picha zaidi  hapa


Shetta akiwa na gari aliyopata nayo ajali aina ya Noha


“Namshuru mungu naendelea vizuri,nipo Babati mjini,nimepata uduma ya kwanza ila bado siko vizuri sana,naomba tuongee baadae”Alisema Shetta.

Shetta alipata ajali wakati anaelekea Babati na gari ya aina ya Noah,jioni ya April 11 2014 baada ya gari kupinduka mara tatu wakati dereva akiwa kwenye jitihada za kumkwepa Punda.

Kwenye gari hilo, Shetta alikua na msaidizi wake pamoja na waandaaji wa show ambapo hakuna aliepoteza maisha isipokua majeraha madogomadogo huku yeye mwenyewe akiumia kichwani na mguuni.

“nashukuru mungu nimetoka salama kweli mungu mkubwa mana nilijua leo ndo mwisho wangu mana ajali ni mbayaaa sanaaaaa…… thnx woteee mlionipa pole tupo pa1.”Shetta alisema baada kusurika na ajali hiyo.
Previous Post Next Post