Picha: Vodacom yatembelea vyombo vya habari nchini kuimarisha uhusiano

Waendeshaji wa kipindi cha Morning Choice kinachorushwa na kituo cha Radio cha Choice FM Baby Kabai (kulia) na Evans Bukuku wakionesha manjonjo kwa Mkuu wa Masoko wa Vodacom Kelvin Twissa na Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Rosalynn Mworia (hawapo pichani) walipotembelea vyombo vya habari vilivyo chini ya Clouds Media Group


Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya New Habari Corporation Hussein Bashe(kulia)akiwaonesha Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia(katikati) na Meneja Uhusiano kwa Umma wa Kampuni hiyo Matina Nkurlu moja ya magazeti yanayochapishwa na kampuni yake wakati maofisa hao walipotembelea ofisi za Magzeti ya Mtanzania zilizopo Sinza jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kukuza uhusiano miongoni mwa kampuni hizo.Wa kwanza kulia ni Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Mtanzania Dennis Msacky

Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia (katikati) na Meneja Uhusiano kwa Umma wa kampuni hiyo Matina Nkurlu wakimsikiliza kwa umakini Mkurugenzi Mtendaji wa New Habari Corporation Hussein Bashe( kulia) akiwalezea mfumo wa uchapaji magazeti. Maofisa hao wa Vodacom walitembelea ofisi za New Habari Corporation zilizopo Sinza jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kukuza uhusiano kati ya kampuni hizo

 Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba akiongea na Mkuu wa Masoko wa Vodacom Kelvin Twissa na Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Rosalynn Mworia. Twissa na Mworia walitembeela vyombo vya habari vilivyo chini ya Clouds Media Group katika ziara ya akwaida ya kuimarisha uhusiano

Muongoza Matangazo wa kituo cha Radio Clouds na Clouds TV Barnabas Madili akionyesha namna kazi ya kuongoza matangazo inavyofanyika wakati Mkuu wa Masoko wa Vodacom Kelvin Twissa(wa kwanza kushoto) na Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Rosalynn Mworia walipotembelea vyombo vya habari vilivyo chini ya Clouds Media Group. Wa tatu kushoto ni Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba
Previous Post Next Post