Picha: Maelfu walivyojitokeza kumzika Mzee Gurumo kijijini kwao alikozaliwa

R.i.p, Maelfu ya wananchi na watu mbalimbali maarufu wamejitokeza kwenye mazishi ya muimbaji mkongwe wa muziki nchini, Mzee Muhidin Gurumo yanayofanyika katika kijiji cha Masaki wilayani Kisarawe, Pwani.


Kwa mujibu wa makamu wa rais wa shirikisho la muziki Tanzania, Samwel Brighton, ushiriki kwenye mazishi huo ni mkubwa ambapo mkuu wa wilaya hiyo amewasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuweka mambo sawa.

Muigizaji wa filamu, Jacob Stephen na mwenzake Dude wakisaidia kuubeba mwili wa Mzee Gurumo

“Ushiriki kwa upande wa dansi watu wote walikuwepo kwasababu kama unavyojua huyu ni baba wa muziki huo na wa maigizo tulikuwa nao wengi tu lakini kwa upande wa kizazi kipya kusema ukweli kwa macho yangu sidhani kama nimeona zaidi ya wasanii 10, sijajua tatizo ni nini lakini ushiriki wao ni mdogo kwakweli,” Brighton amekiambia kipindi cha Power Jams cha East Africa Radio.

Profesa Jay ni miongoni mwa wasanii waliohudhuria mazishi hayo

Wananchi wakimzika Mzee Gurumo katika kijiji cha Masaki, Kisarawe

Mzee Gurumo alifariki Jumapili baada ya kulazwa kwenye hospitali ya taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam. Amewahi kuimba na bendi mbalimbali zikiwemo Kilwa Jazz Band, Nuta Jazz Band, Mlimana Park, Safari Sound na baadaye Msondo Ngoma.




Previous Post Next Post