Mapacha maarufu zaidi barani Afrika, Peter na Paul Okoye wa kundi la P-Square la Nigeria, wote wamepata majiko kwa kufunga ndoa za kimila. Mapacha hao walioa katika muda tofauti ambapo Peter ndiye aliyeanza mwaka jana kwa kufunga ndoa na Lola Omotayo (mkubwa zaidi kiumri kumzidi Peter) aliyekuwa tayari amezaa naye watoto wawili na Paul kufunga yake mwaka huu na Anita Isama aliyekuwa amezaa naye mtoto.
Tungependa utuambie, nani mrembo zaidi kati ya Lola na Anita?