Nash MC aweka wazi kuwa anamzimia Meninah "mkimuona mwambieni"

Unaweza kuichukulia kivyovyote lakini maandishi ya member wa Tamaduni Music, Nash MC yameeleza wazi kuwa anamzimia mrembo na mwimbaji wa kundi la Shosteez, Meninah la Diva.



Comment ya Nash MC aliyoiweka kwenye post ya Jabir Saleh aka Kuvichaka aliyokuwa ameweka kwenye ukurasa wa Facebook akiwa na Dayna Nyange ambaye atakuwa mkali wa The Jump Off kuanzia wiki ijayo, ilikuwa na ujumbe wa wazi kwa mtangazaji huyo.

“Siku ukimhoji menina nistue maana mamzimia kweli.” Aliandika Nash MC.

Hata hivyo, ujumbe huo haukuishia kwa Kuvichaka na akaupeleka kwa watu wengine ambao wanaweza kukutana na Meninah au wale ambao walidhani ametereza tu kuandika kwa uwazi.

“Hilo lipo wazi na mkimuona mwambieni.” Alisisitiza Nash MC.

Rapper huyo wa Naandika alijitoa kwenye lawama binafsi na kuchombeza kiutani kuwa kilichomsukuma na upendo. “Sio mm ni sababu ya mapendooooooo!”
Previous Post Next Post