Linex kuacha kuvaa mlegezo ili asiendelee kumkwaza mama yake Roma na wengine

Wiki kadhaa zilizopita, Roma Mkatoliki alieleza kupitia kipindi cha Bongo Dot Home cha 100.5 Times Fm kuwa mama yake ni shabiki mkubwa wa nyimbo za Linex lakini uvaaji wake wa suruali ‘mlegezo’ una mkwaza sana.

Jumamosi iliyopita kupitia kipindi cha Bongo Dot Home, Linex alieleza kuwa analifahamu hilo kutokana na kuwa rafiki wa karibu wa Roma Mkatoliki na hivyo alishaambiwa na mama yake Roma na alimuahidi kubadilika.



“Na nilimpromise…unajua mimi nina itikadi moja, mama yako wewe ni mama yangu mimi. Mama yako wewe is my mom too. Kwa hiyo mama yako wewe akiniambia jambo I feel the same.” Amesema Linex.

“Kwa hiyo kwanza kabisa unajua nilimpromise bi mkubwa kwamba I will change. Kwa sababu hiyo pia nimekuwa nikigombana na mama yangu mzazi. Unajua itikadi za mama zetu zinafanana, it’s the same issue my man. Yaani ma-mama hawatofautiani, mama yako na mama yangu wanapenda vitu same.” Ameongeza Linex.

Mkali huyo amefafanua kuwa kutokana ukaribu uliopo kati yake na rapper wa ‘KKK’ humuita kwa jina lake halisi la Ibrahim badala ya Roma na yeye humuita Sunday.

“Kwa hiyo big shout out kwa mama yake Ibra ambaye ni mama yangu pia kwa kukubali nachokifanya, au vipi bana…na pia nimpromise kwamba I will change, anipe time kwamba tayari nishakuwa mtu mzima kwa hiyo nataka kuchange vitu kibao na nini. Na moja kati ya vitu ambavyo vitaingia kwenye protocol yangu ya kuchage ni hiyo kitu ambayo mama yake Roma alicomplain ambaye ni mama yangu pia. Kwa hiyo nipewe tu time kidogo, sometime good inakuja soon…very very soon.”


Credit:Timesfm
Previous Post Next Post