Kukataa kwa Jay Z kuwa mpambe wa Kanye West kwenye harusi yake kumetia dosari urafiki wao

Utajisikiaje pale rafiki yako wa damu anapokataa kuwa mpambe wa harusi yako ama kuhudhuria kwa sababu rahisi kama ya kutopenda kuonekana kwenye TV?

Kanye West na Kim Kardashian wanajiandaa kufunga ndoa wiki chache zijazo jijini Paris, Ufaransa, lakini mgeni mmoja muhimu kwenye harusi hiyo hatokuwepo, rafiki wa Kanye, Jay Z. Jay Z alitosa ombi la Kanye kuwa mpambe wake wa harusi kwa sababu ambayo kwa wengi inaweza kuonekana nyepesi na ya kipuuzi. Hov hataki kuonekana kabisa kwenye show ya Keeping Up with the Kardashians!



“Of course, Kanye alimuomba Jay awe mpambe wake kwenye harusi. Lakini Jay alikaa ombi hilo,” mtu wa karibu ameuambia mtandao wa Hollywood life. “Jay hakutaka kuhusishwa kwenye reality show ya Kardashian. Kanye alimuambia Jay anaelewa kwanini amekataa, lakini bado aliumia sana.”

Ni wazi kuwa rafiki yako mliyefanya mambo mengi pamoja anapokutosa kwenye siku yako muhimu kama hiyo, ni lazima utaumia na ni ngumu kuelewa kwanini Jay kukataa hata kama alikuwa na sababu zake. Jay Z na Kanye West wameshirikiana kwenye album ya pamoja na wanajulikana jinsi walivyo karibu kwenye muziki.

Pia familia Kardashian lazima ichukulie kitendo hicho kwa shingo upande. Hiyo itamaanisha kuwa Jay Z haipendi familia hiyo au hajapenda Kim awe na mke wa rafiki yake Kanye.



Katika hatua nyingine ni kwamba mtandao wa Page Six umedai kuwa jarida la Vogue lenye kava la Kim Kardashian na Kanye West linaweza kuuza kati ya kopi 300,000 na 400,000 na hivyo kuzidi issue za jarida hilo za Beyonce na Michelle Obama ambalo la Beyonce liliuza kopi 355,000 na Obama kopi 300,000.
Previous Post Next Post