Ben Pol Kufanya show Nchini Ujerumani, ni mara yake ya kwanza kufanya show ya kimataifa

Mkali wa R7B Bongo Ben Pol baada ya kuvuna mafanikio kadhaa kupitia muziki wake ikiwa ni pamoja na kuzoa tuzo hapa nyumbani, na video yake ya ‘Jikubali’ kuwa ya kwanza kuchezwa Channel O, mwimbaji wa ‘Unanichora’ Ben Pol amepata shavu la kwenda nchini Ujerumani kufanya show mwisho wa mwezi huu.


‘Team Ben Pol is gonna be perfoming in München on 30th April 2014 #Twendesasa #Ready???’, hiyo ni status ya Ben Pol kupitia ukurasa wake wa Facebook.


Ben Pol ambaye ameachia album yake mpya siku chache zilizopita online, ameiambia Bongo 5 kuwa show hiyo ya Ujerumani ndio ya kwanza ya kimataifa kuwahi kuipata, japo atakapokuwa huko anatarajia kufanya show zingine katika miji iliyoko karibu na anakoenda japo kwasasa hiyo ya Munchen ndiyo iliyothibitishwa.

Ameongeza kuwa waandaaji wa show hiyo walimtafuta takribani miezi mitatu iliyopita na wakawa bado hawajafikia makubaliano hadi kipindi hiki.


Previous Post Next Post