Member wa zamani wa kundi la Wakilisha, Witness ‘Witnesz’ Mwaijaga amepanga kuendesha semina maalum kwa wadau wa muziki Tanzania kuhusu jinsi ya kufanya biashara ya muziki nchini bila kutegemea sana radio na Tv.
Witness amekiambia kipindi cha The Jump Off cha 100.5 Times Fm kuwa baada ya kutoka marekani alikuwa na mpango huo lakini alishindwa kutokana na kukosa wadhamini kwa muda huo ili kufanya semina kubwa.
Hata hivyo, baada ya kukaa na watu wake wameamua kuendesha semina kwa kuchukua watu watano tu kwa wiki ili kufikisha kile alichokuwa amekikusudia toka awali.
“Nilitaka nirudi kufanya hiyo program, ila hiyo program huwezi ukafanya pasipokuwa na sponsors, so nikawa nimeangalia kama nitapata sponsors. Asilimia kubwa ya nilichokuwa nafanya, nilikuwa nataka kufundisha watanzani au watu ambao wanataka kufanya biashara ya muziki wafanye seriously kama biashara na vilevile niwaelezee jinsi gani ya kuweza kufanya pasipotegemea mfumo uliozoeleka nikimaansisha radio na TV. Na the same time waweze kufanya vitu gani kwa ajili ya kuwa wanamuziki wa kitaifa hadi kuwa wa kimataifa.” Ameeleza.
Rapper huyo wa kike amesema tayari wameshakubaliana na
semina hiyo itaanza May 5, mwaka huu.
“Project yenyewe tunaanza tarehe 5 mwezi wa 5, na tayari kuna watu wapo na hatuchukui watu wengi. Kwa wiki moja tunachukua watu watano tu kwa sababu tunataka watu waweze kuendelea.” Amesema Witness.
Amefafanua kuwa semina hiyo inawakaribisha wadau wote wa muziki wanaohitaji kama watayarishaji wa muziki, wasanii, mameneja, na watangazaji wa radio na television.
Msikilize hapa akieleza kiundani:
Source:Timesfm

Tags:
Entertainment