Audio: Ommy Dimpoz aeleza alichojifunza kwa Mzee Gurumo na anavyomkumbuka, ni funzo kwa wasaniiz aeleza alichojifunza kwa Mzee Gurumo na anavyomkumbuka,

Ommy Dimpoz ni mmoja kati ya wasanii wakubwa wa bongo flava ambao waliwahi kutumbuiza kwa kurudia moja kati ya nyimbo za marehemu mzee Muhidin Gurumo katika jukwaa la KTMAs 2013 na kuutendea haki.

Tovuti ya Times Fm imezungumza na Ommy Dimpoz ambaye ameeleza jinsi ambavyo anamkumbuka gwiji huyo wa muziki wa dansi.

Ameeleza kuwa anakumbuka tangu akiwa mtoto alikuwa na mama yake mkubwa na mjomba wake ambao walikuwa wanafanya kazi katika shirika la JUWATA hadi lilipobadilishwa na kuitwa OTTU na yeye alikuwa na nafasi ya kuingia bure kwenye ukumbi waliokuwa wakiimba akina mzee Gurumo na hivyo alikuwa ni shabiki wao anaewafuatilia tangu enzi hizo.

Moja kati ya vitu anavyovikumbuka ni msimamo aliokuwa nao mzee Gurumo katika Bendi yake.

“Kiukweli naweza kusema Tanzania imepoteza hazina. Halafu ni mmoja kati ya wasanii wenye msimamo kwa sababu nakumbuka kwa miaka ile tulikuwa tunaona bendi wasanii wanahama sana, leo huyu kaenda huku kaenda huku. Kwa sababu pale Msondo nakumbuka kulikuwaga kuna marehemu Moshi William, Marehemu Hassan Momba, marehemu Mwanyiro na Hassan Bichuka. Lakini wengine walikuwa wanahama mzee anabaki kama ngao ya Msondo.” Ameeleza Ommy Dimpoz.






Amesema hiyo ilimfanya ajifunze kutoka kwake kuhusu msimamo na nidhamu ya kazi kwa kuiongoza bendi hiyo kwa kipindi kirefu.

Kikubwa ambacho hadi leo atabaki akikitumia kutoka kwa Mzee Gurumo ni ule utambulisho binafsi katika kazi ya muziki.

“Kitu ambacho kikubwa najifunza ni ile Identity yake aliyojitengenezea ambayo wasanii wengi imekuwa inatupa tabu hususani wa muziki wa sasa hivi kutengeneza ile kitambulisho chako kiasi kwamba mtu akikusikia hata usiku wa manane anajua kabisa huyu ni Gurumo.

“Lakini ukiangalia kwa vitu vingine ndo kama hivyo kwamba ili u-succeed katika muziki lazima uwe mvumilivu kidogo. Naweza kusema yeye anaweza akawa ni mtu ambaye alifanya kazi kubwa labda hakufaidika sana na muziki huenda kulingana na wakati ambao umekuwa kidogo tofauti. Sasa hivi wanamuziki wa bendi anaweza akanunuliwa kutoka Twanga akaenda bendi nyingine akalipwa hela nyingi kidogo tofauti na wao jinsi ilivyokuwa.”

Mzee Gurumo alifariki dunia Jumapili iliyopita katika hospitali ya taifa ya Muhimbili alikokuwa akipata matibabu ya ungonjwa wa moyo. Mwimbaji huyo mkongwe alifariki akiwa na umri wa miaka 74.

Msikilize hapa Ommy Dimpoz kwa akieleza kwa urefu:


Source:timesfm
Previous Post Next Post