Samsung kuinunua selfie ya Ellen DeGeneres kwa dola milioni 3, yadai haikuwa ‘stunt’

Kampuni ya simu ya Samsung imesema selfie maarufu iliyochukuliwa kwenye Oscars ilikuwa ni surprise kwa kila mtu baada ya kuibuka ripoti kuwa ilikuwa imepangwa kama stunt ya kimasoko ya kampuni hiyo iliyokuwa imedhamini tuzo hizo.




Kampuni hiyo ya Korea Kusini iliyopata shavu la nguvu baada ya Ellen DeGeneres kutumia simu ya Samsung kuchukua picha hiyo imesema itatoa dola milioni 3 kwa host huyo wa Oscars atakayezipeleka kwenye charity atakazochagua yeye. Samsung ilikuwa imedhamini show hiyo kwa kituo cha ABC kilichorusha live matangazo hayo na ililipa dola milioni 20.

The Wall Street Journal lilidai kuwa wakati wa rehearsals maofisa wa Samsung walimfundisha Ellen DeGeneres jinsi ya kutumia Samsung Galaxy. Hadi sasa picha hiyo imeshakuwa retweeted kwa zaidi ya mara milioni 3.30.

Previous Post Next Post

Popular Items

Magazetini Ijumaa ya Tarehe 23/8/2013