Raha wazindua rasmi huduma ya internet kupitia mkongo wa fiber (fiber optic network)

Kampuni ya utoaji huduma ya internet nchini ya Raha, leo imezindua rasmi huduma ya utoaji wa internet kwa kutumia mkongo uliochimbiwa chini wa fiber optic network.




Mwenyekiti Mtendaji (CEO) wa Raha, Aashiq Shariff akiongea na waandishi wa habari

Akiongea na waandishi wa habari, Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni hiyo, Aashiq Shariff amesema kampuni hiyo ilifanya uwekezaji mkubwa kuweza kufikia hatua hiyo iliyowachukua zaidi ya miaka miwili.

“Jitihada zetu siku zote zimekuwa ni uwekezaji wa nguvu katika miundo mbinu na teknolojia na kuifanya Tanzania kuwa nchi muhimu kwenye mawasiliano. Tunaamini Tanzania ipo sehemu nzuri, nadhani tuna mandhari maridhawa na nchi maridhawa na kuwa nchi muhimu si tu kwenye teknolojia bali pia mambo mengine,” amesema Shariff. “Hapa raha tunaamini fiber optic network ni mustakabali wa teknolojia, tunaamini kwamba ni kitu kikubwa kijacho,” aliongeza.



Chief Commercial Officer wa Raha, Akash Karia akifurahia jambo kwenye mkutano huo

Shariff amesema teknolojia hiyo inawezesha kusafirishwa kwa taarifa kwa kutumia mwanga. “Hii itakuhakikishia si tu kuwa unaungwanishwa na internet lakini sauti yako, data zako na vingine navyo vinaungwanishwa kwenye internet.”

Mkuu wa Masoko wa Raha, Reena Pandya akiwa kwenye mkutano huo
Ameongeza kuwa fiber inatumika si tu katika kupata internet bali pia inaweza kutumia kwa kazi za utangazaji, sauti na video na kwamba mkongo huo tayari umeunganishwa katika maeneo yote ya jiji la Dar es Salaam, Zanzibar na Arusha. Kwa upande wake Ofisa Mkuu wa Teknolojia kwenye kampuni hiyo, Nyangu Meghji amesema kuwa teknolojia hiyo ilianzia nchini Marekani zaidi ya miakan 30 iliyopita na uwezo wake ni mkubwa ukilinganisha na mtandao usiotumia waya (wireless).

Ofisa Mkuu wa Teknolojia kampuni ya Raha, Nyangu Meghji akitoa ufafanuzi kuhusiana na umuhimu wa fiber

“Unapokuwa kwenye fiber unakuwa na rasilimali isiyo na mwisho kwasababu upo ndani ya kioo ambacho kitakusafirisha kwa mwende wa mwanga,” alisema Meghji.

Kampuni hiyo imesema kutokana na kuanza kutumia teknolojia ya fiber, huduma zake za internet zitakuwa za uhakika na wateja watapata internet yenye spidi kubwa zaidi.
Previous Post Next Post