Miss Tanzania 2013, Happiness Watimanywa hana mpango wa kuonekana kwenye video za wasanii wa bongo flava ama filamu kama baadhi ya washiriki wa shindano hilo.
Happines Watimanywa ameiambia Times Fm kuwa yeye binafsi hana mpango wa kuingia kwenye video za wasanii kama video vixen/video queen kwa kuwa hana kipaji hicho na hana mzuka wa kuonekana kwenye tasnia hizo.
“My passion is not acting, I’m not a very good actress na kama unataka kuwa kwenye video inabidi uwe convincing sana. Yaani inabidi uweze kuigiza, na mimi sio muigizaji mzuri kwa hiyo it’s not something ambayo nataka kukifuatilia.” Amesema Happiness.
Katika hatua nyingine, mrembo huyo amezungumzia kile ambacho wengi wanasema kuwa mashindano ya kumtafuta Miss Tanzania yamepungua umaarufu.
Happiness anaamini mashindano hayo bado ni maarufu kwa kuwa bado kuna wasichana wengi wanaotaka kuingia kwenye mashindano hayo.
“Nadhani mashindano bado ni maarufu sana kwa sababu unakuta wasichana wenyewe ambao wanataka kushiriki unakuta ni wengi sana. Na nakutana na watu wengi sana ambao wananiambia Happy nifanyeje ili na mimi niingie kwenye hii kitu?’ Au unakuta labda kwenye social networks kuna watu wanafuata sana.” Happiness ameeleza.
Mrembo huyo wa Tanzania amedai kuwa inawezekana watu hawaongelei mitaani shindano hilo lakini kwenye mitandao ya kijamii shindano hilo linazungumziwa.
Msikilize hpa chini akiongea..!
Source:Timesfm

Tags:
celebrity News