Lady Gaga alitumia tsh bilioni 4.8 kwa ajili ya jukwaa, kwa sasa adai amepigika

Lady Gaga alimwacha mdomo wazi baba yake baada ya kumwambia amepigika kutokana kumwaga mamilioni ya dola kutengeneza jukwaa kwaajili ya ziara yake ya mwaka 2009 ya Monster’s Ball.



Muimbaji huyo anadai alitumia dola milioni 3 (zaidi ya shilingi bilioni 4.8 za Tanzania) kutengeneza jukwaa ili kuwapa mashabiki wake tumbuizo la live la kipekee na ili kumfurahisha promota muhimu.

Kwenye makala mpya itakayoonekana kwenye US TV wiki hii Gaga anasema: Nilikuwa nimeishiwa kabisa wakati wa show. Nilikuwa na dola milioni 3 benki na zote nilizotupa kutengeneza jukwaa.” Promota aliyetaka kumfurahisha ni Fogel wa Live Nation anayesimamia ziara za U2 na za Madonna. Hata hivyo, jitihada hizo zililipa kwakuwa Fogel alifurahishwa na kujituma kwa Gaga na akakubali kuongoza ziara yake iliyofuata ambayo iliingiza dola milioni 220.

“Kila mtu alisema isingetokea. Nakumbuka Fogel alinipigia simu na kuniambia ‘tunataka kufanya hii’ na akawafanya Live Nation waniandikie cheki ya dola milioni 40. Ilibadilisha maisha yangu na maisha ya familia yangu yote.”
Previous Post Next Post