Kala Jeremia Baada ya Kutokuchaguliwa kuwania KTMA mwaka huu, Azungumza haya

Mshindi wa tuzo kadhaa za muziki za Tanzania (KTMA 2013), Kala Jeremiah ambaye mwaka huu jina lake halikutajwa katika vipengele vyote vya kuwania tuzo hizo ametoa mtazamo wake kuhusu kutotajwa kwake.

Rapper huyo wa Rock City Mwanza amesema kuwa moyo wake uko sawa na anaona kila kitu kiko sawa na kwamba hana hata swali.



“Yaani mimi sijui nikoje, nimezaliwa tofauti sana nadhani na binadamu wengine. Yaani ni mtu fulani wa ajabu sana, naonaga kila kitu kiko sawa. Moyo wangu uko tofauti sana, sina tatizo lolote yaani sijui nikwambieje…yaani niko very comfortable na naona ni sawa kabisa sina swali sina chochote kwenye moyo wangu niko vizuri. Naona ni Mungu aliniumba vizuri sana hivi nilivyo kwa sababu kila kitu nakichukulia fresh.” Kala Jeremiah aliongea

Ameeleza kuwa anaona watu walioingia walistahili kuingia na kwamba hata mwaka jana hakuwa anatarajia kuingia kwenye vipengele hivyo na hata kushinda, kwa hiyo hata mwaka huu pia alikuwa hatarajii chochote.

“Ndio maana nilipotajwa mwaka jana nikashtuka na hata nilipopata tuzo pia nikashtuka. Yaani kila kitu mi nadhani kinatakiwa kije chenyewe kwa sababu ukikifikiria kitu…mi naona hata kukifikiria kitu na kupanga eti itakuwa hivi au itakuwa hivi, no. Sidhani kama hiyo ni njia sahihi, njia sahihi mimi naona ni kufanya kazi nzuri na kuacha watu wafurahi na kazi zako.” Ameongeza rapper huyo wa Wale Wale.

Kala ameeleza kuwa hata wakati anashiriki mashindano ya BSS hakuwa na wasiwasi wa kuendelea ama kutoendelea na mashindano kwa kuwa kwake yeye huona kila kinachotokea katika hali hiyo ni sawa.

Wimbo wa Dear God uliotayarishwa na Dee Classic ulimpa tuzo tatu muhimu mwaka jana ikiwa ni pamoja na tuzo kubwa ya wimbo bora wa mwaka. Alishinda pia tuzo ya msanii bora wa hip hopakiwabwaga Fid Q, Joh Makini, Profesa Jay na Stamina.

Kala aliitoa tuzo ya wimbo bora wa hip hop na kumkabidhi mama yake Albert Mangwea kwa heshima na kumuenzi rapper huyo aliyefariki May 28 mwaka jana nchini Afrika Kusini.
Previous Post Next Post