Huyu ndiye Mpenzi mpya wa Shilole,Ni Chipukizi katika BongoFleva

Staa anayekimbiza kwenye filamu na muziki wa mduara, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ au ‘Shishi’ ameibuka katika penzi jipya na bwana mdogo anayechipukia katika muziki wa Bongo Fleva, Nouh Mziwanda,


Shilole kwa sasa hasikii wala haoni kwa Nouh pamoja na kwamba wawili hao wanaonekana kuwa na tofauti kubwa ya kiumri , Shilole akionekana kuwa mkubwa zaidi ya Nouh.


Shilole akiwa na Nouh Mziwanda.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, Shilole kwa sasa hasikii wala haoni kwa Nouh pamoja na kwamba wawili hao wanaonekana kuwa na tofauti kubwa ya kiumri , Shilole akionekana kuwa mkubwa zaidi ya Nouh.
“Ni kweli ninatoka na Shilole ni mpenzi wangu na sidhani kama nitakuja kuachana naye maana tunapendana sana na nimevutiwa na mavituz yake,” alisema Nouh.
Kuhusu tofauti ya umri wake na ule wa Shilole, Nouh alisema umri huwa haumati katika mapenzi.

“Mapenzi ni mapenzi na umri utabaki kuwa namba tu, ni vyema  mtu ukaongozwa na hisia zako kuliko kuhofia umri wa mtu ndiyo maana miye ninakula vinono,” alisisitiza.
Pia, Nouh alisema hakutarajia kukubaliwa na  Shilole baada ya kumtokea walipokutana  katika  studio moja jijni Dar na sasa wamekolea kwenye penzi motomoto.

“Nampenda Shishi, nafanya kila njia nimshawishi awe mke wangu wa ndoa,” aliongeza.
Hata hivyo, Shilole alipozungumza na waandishi wetu alipatwa na  kigugumizi kukubali uhusiano wake wa kimapenzi na kinda huyo wa Bongo Fleva.




Shilole alisema Nouh ni rafiki yake kama walivyo marafiki zake wengine.
Waandishi wetu walipomuonesha picha zao walizokuwa wamekaa katika mikao ya  kihasarahasara, Shilole aliangua kicheko na kisha akasema:

“Mh! Sina la kuwajibu kama picha zinasema mimi na Nouh ni wapenzi haya.”  
Hii siyo mara ya kwanza kwa Shilole kuripotiwa kutoka na Serengeti Boy

Chanzo:Globalpublishers
Previous Post Next Post

Popular Items

EXPENSIVE THING OF THE DAY

New Music: Blue - Pesa