Fast & Furious 7 kuendelea kurekodiwa mwezi April, ni baada ya kusimama ‘production’ miezi 4 baada ya kifo cha Paul Walker

Ikiwa ni takribani miezi mitatu imepita toka star wa filamu ya Fast & Furious, Paul Walker apoteze maisha mwishoni mwaka jana (2013) katika ajali ya gari, filamu ya Fast & Furious 7 imepangwa kuendelea kurekodiwa kuanzia mwezi ujao.





Watengenezaji wa Fast & Furious 7 walisimamisha production ya filamu hiyo baada ya kifo cha Walker kilichotokea Novemba 30, 2013 , ili kutoa nafasi kwa waigizaji wenzake kushiriki katika msiba wa rafiki yao pia na watengenezaji wenyewe kupata muda wa kupanga upya script ya filamu hiyo kutokana na kuwa Walker alikuwa ni mmoja wa waigizaji waliokuwa wanahusika.

Kwa mujibu wa Hollywood Reporter, production itaendelea kuanzia tarehe moja mwezi ujao (April) huko Atlanta, Marekani huku ikiwa inaaminika kazi iliyokuwa imesalia ili filamu ikamilike ni ya wiki sita hadi nane.

Pamoja na kufanya marekebisho katika script, Universal Picture wamethibitisha kuwa Walker ambaye pia alikuwa ameshoot baadhi ya scenes kabla ya mauti kumkuta, ataendelea kuonekana katika Fast & Furious 7 japo kuwa wamebadilisha kidogo role yake.

Mpaka wakati wa kifo cha Walker tayari asilimia 60 ya filamu hiyo ilikuwa tayari imekwisharekodiwa.

Fast & Furious-7 imepangwa kutoka April 10 mwakani (2015).

Previous Post Next Post