Ni juzi tu hapa vyombo vya habari mtandaoni viliandika kuwa Drake na Rihanna ni wapenzi na wameamua kuuchukulia uhusiano huo serious zaidi. Na sasa vyanzo vinadai kuwa wawili hao wamezinguana tena – kisa Chris Brown. Chanzo cha uhakika kimeuambia mtandao wa Urban Islandz kuwa Rihanna amekuwa akiwasiliana na Chris Brown ambaye hata hivyo kwa sasa yupo jela.
“Robyn bado anampenda sana Chris na Drake alishtukia kuwa amekuwa akiwasiliana naye,” chanzo kilisema. “Siku moja alimsikia akiongea na Chris na kumfokea lakini Riri alikanusha kuwa na uhusiano na Chris. Kisha aligundua kuwa Rihanna na Chris wamekuwa wakitumia jumbe za mapenzi na kumfanya akasirike kiasi cha kuamua kuvunja tena.”
Chanzo hicho kimedai pia kuwa Karrueche Tran alimpiga chini Brown alipogundua kuwa alikuwa akimtumia sms za mapenzi Rihanna.