Mwimbaji wa bongo flava ambaye pia ni muigizaji wa filamu za kitanzania, Snura amesema kuwa amepunguza viuno kwenye video za nyimbo zake kutokana na kukosolewa na hata kutolewa kwenye baadhi ya vipengele vya KTMA.
Akiongea katika kipindi cha Mitikisiko ya Pwani cha 100.5 Times Fm na Dida Shaibu, Snura ameeleza kuwa hata kabla BASATA hawajapiga stop ushiriki wa nyimbo zake kwenye kinyang’anyiro chaKilimanjaro Tanzania Music Awards alikuwa ameshabadilika kwa kuwa tayari video yake ya ‘Nimevurugwa’ ilikuwa imefungiwa.
“Tayari mimi nimeshabadilika kabla hata hatujafika huko kwenye Kili kwa sababu ilifungiwa muda kidogo kabla mambo ya Kili hayajaingia. Na wimbo wangu wa Ushaharibu nilikuwa nimeshafanya video pia, unajua nilikuwa nimeshafanya video ya Ushaharibu. Wimbo wangu wa Ushaharibu ukitoka watu watajua ni jinsi gani nimeweza ku-change.” Amesema Snura.
Ameeleza kuwa sio kwamba kwenye ‘Usiharibu’ hakutakuwa tena na uchazaji ule wa kukata viuno baliatapunguza kidogo.
“Kweli kwenye video sio kwamba hakuna kabisa kiuno ila nimepunguza. Nilichokifanya nimepunguza, nimeacha viuno ambavyo ninauhakika kwamba siwezi kufungiwa jamani. Sijakatika kama kwenye Nimevurugwa. Wakati nafanya wimbo wa Nimevurugwa sikuhisi kama naweza nikafungiwa kiukweli. Laiti kama ningejua nisingeweza kufanya vile. Nilichukulia kama ni ubunifu na utundu wangu ndio maana nikafanya vile.” Snura ameeleza.
Hata hivyo, amedai kuwa kuna mashabiki wake ambao wangependa kuona anacheza kama alivyokuwa akicheza zamani hivyo ataendeleza mchezo huo kwenye shows zake atazofanya kwenye kumbi.
“Najua nina mashabiki wale ambao wanakuwa wanapenda sana viuno, naomba wanivumilie kwenye video hawataweza kuona viuno kama vile ambavyo wao wanavihitaji, watakutana tu na kiuno cha kawaida. Ila kwa wale ambao wanaoweza kufika kwenye show zangu…kwenye show naweza kujiachia kama kawaida.”
Amefafanua kuwa havitakuwa viuno vitakavyokiuka maadili ya kitanzania na kuongeza kuwa yeye binafsi hapendi kuonesha jinsi anavyoweza kukata viuno.
“Lakini toka naanza kwenye muziki, nimefanya research nisipokatika…unajua kuna show nafanya nimesimama, lakini mashabiki wanalalamika wanataka kunipiga ‘sio wewe yaani wewe sio Snura kabisa, tunataka miuno’. Mimi nimfanya biashara sina jinsi inabidi nikatike ili niwafurahishe wateja wangu ili waweze kujaa kwenye show ili waweze kuingia kwenye show ili waweze kunikubali..mimi natafuta riziki.”

Msikilize hapa: