Video: 50 Cent atoa video ya wimbo mpya ‘The Funeral’

Ikiwa ni siku moja toka atangaze kusaini dili mpya na kampuni ya usambazaji Caroline/Capito/UMG, na kujitoa Interscope Records, Aftermath Entertainment na Shady Records, rapper Curtis Jackson aka 50 Cent hajataka kupoteza muda kwa kuamua kuachia wimbo na video mpya.



Wimbo huo unaitwa Mazishi ‘The Funeral’, ambayo inaonekana ‘kama’ part two ya wimbo wake ‘50 Bars’ uliotoka katika compilation yake ya mwaka 2002.

Video hiyo 50 aliitoa kwa mara ya kwanza jana kupitia Forbes ambao walifanya naye interview ya kwanza toka taarifa juu ya kusaini kwake dili mpya ya usambazaji pamoja na kujiondoa Interscope ifahamike.

Tazama Video hapa chini



Katika Interview hiyo Fiddy alielezea uhusiano wake na maswahiba wake Dr. Dre na Eminem baada ya kuchukua maamuzi ya kujitoa:

“I’m a special case and situation, It’s also because of the leverage of having the strong relationships with Eminem and Dr. Dre. They don’t want to me to be uncomfortable. They value our friendship to the point that they would never want [to jeopardize] it over that little bit of money.”
Previous Post Next Post