UN yaitaka Vatican kuondoa baadhi ya mapadri.

Kamati ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imetoa dai la kipekee la kutaka Vatican iondoe mara moja mapadri wote wanaoshutumiwa kwa kunyanyasa watoto kingono na kuwakabidhi kwa mamlaka za sheria.

Kamati hiyo Jumatano imeitaka ofisi ya Vatican (Holy see) kutangaza unyanyasaji wa maelfu ya watoto na kukabidhi nyaraka zao juu ya suala hilo.




Kamati hiyo inasema kwamba ina wasi wasi mkubwa kwamba kanisa halijatangaza ukubwa wa makosa yaliofanyika na haijachukua hatua stahili za kupambana na kesi hizo na limechukua sera ambazo zinaendeleza vitendo hivyo bila kuwa na uwajibikaji wowote.

Huu ni ujumbe wa wazi  kuliko yote kuwahi kutokea kutoka kamati hiyo kuelekea Vatican kuhusiana na unyanyasaji wa kingono wa mapadri kwa  watoto. Mwezi uliopita maafisa wa Vatican walihojiwa kwa muda mrefu na wajumbe wa kamati hiyo.

Vatican ilijibu Jumatano ikitoa taarifa kwamba ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa itapitiwa kwa kina na kuongeza kwamba inaona sehemu ya ripoti hiyo kama jaribio la kuingilia mafundisho ya kanisa katoliki juu ya heshima ya binadamu na katika kutumia uhuru wa kidini. 

Papa Francis aliunda tume mwezi Desemba kuchunguza kesi zote zilizoripotiwa za unyanyasaji huo.

Chanzo:Voa.com
Previous Post Next Post

Popular Items