Msanii wa filamu Mahsein Awadh Said maarufu kama ‘Dk. Cheni’ ameitupia lawama Bodi ya Filamu Tanzania (TFB) baada ya kuzuia filamu yake ‘Nimekubali kuolewa’ kwa madai kuwa imekiuka maadili ya Kitanzania.
Akizungumza na Global publishers, DK. Cheni alisema moja ya kigezo ambacho bodi hiyo imekitumia kuzuia filamu hiyo ni pamoja na muonekano wa bango la filamu hiyo ambalo linamuonesha msanii huyo akiwa amevaa vazi la shera huku akiwa amejiremba kwa madai kuwa ni kuchochea ushoga jambo ambalo msanii huyo amelipinga vibaya.
“Eti ushoga wangu uko kwenye kujiremba sana, hakika wamenionea sana, lengo letu ni kuonya na kukemea vikali vitendo vya ushoga na ndoa za jinsia moja, huwezi kuelimisha bila kuonesha madhara yake kwa vitendo kama ilivyo ndani ya filamu hiyo,” alisema.
“Lakini, ndani ya filamu hiyo, kuna kipande ambacho kinaonesha kiongozi wa serikali akikemea kitendo hicho, sasa hapo ushoga wangu uko wapi? Kuvalia shera kwenye kava? Siyo sahihi,” alisema Dk. Cheni.

Source: Global Publishers