Barcelona yaifunga Manchester City 2-0

Timu ya Barcelona imeibuka na ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Manchester City katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya iliyomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Etihad, Manchester!


 Messi akifunga bao la kwanza kwa Barcelona.
Beki wa Man City, Martin Demichelis akimchezea Messi rafu iliyopelekea penalti na kadi nyekundu.

Mabao ya Barcelona yamewekwa kimiani na Lionel Messi kwa mkwaju wa penalti dakika ya 54 baada ya kuangushwa eneo la hatari na beki wa Man City, Martin Demichelis aliyepewa kadi nyekundu.

Bao la pili limefungwa na Dani Alves dakika ya 90 ya mchezo na kuipa ushindi wa bao 2 Barcelona.

Martin Demichelis akizawadiwa kadi nyekundu.


Wachezaji wa Barcelona, Fabregas na Iniesta wakimpongeza Messi baada ya kufunga bao la kwanza.

Previous Post Next Post

Popular Items