Atletico yashikilia nafasi yao adimu Madrid wanafuata

Atletico Madrid imekalia usukani peke yao kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa msimu huu wakati walipoichakaza Real Sociedad 4-0 Jumapili. 

David Villa, Diego Costa, Miranda na nyota mpya Diego alifunga bao la nne na kuiweka Atletico kileleni wakiwa mbele kwa pointi tatu kwa Barcelona, baada ya mabingwa hao kupoteza mwelekeo wiki hii.



Barcelona walichapwa 3-2 na Valencia Jumamosi, kuongoza kwa Atletico kumevunja utawala wa Barca na Madrid wakati wakiwa kwenye harakati za kusaka taji la kwanza tangu 1996.

Madrid wamelingana kwa pointi na Barcelona baada ya kulazimisha sare 1-1 na Athletic Bilbao katika mchezo ulioshuhudia Ronaldo akipewa kadi nyekundu zikiwa zimebaki dakika 15 baada ya kumchapa kibao cha usoni Carlos Gurpegi.



MILAN

Juventus ilipata ushindi mnono wa mabao 3-1 dhidi ya mahasimu wake Inter Milan na kuendelea kuongoza
ligi kwa tofauti ya pointi tisa kileleni.

Stephan Lichtsteiner, Giorgio Chiellini na Arturo Vidal walifunga mabao ya Juventus kabla ya Rolando kufunga bao la kufutia machozi kwa Inter.

Kikosi cha Antonio Conte kimeendelea kuwaacha Roma katika nafasi ya pili ambao mchezo wao dhidi ya Parma ulisitishwa dakika ya nane baada ya uwanja kujaa maji.

Juventus pia ipo mbele kwa pointi 15, kwa Napoli waliopokea kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa Atalanta, huku nyota wao wa zamani German Denis akifunga mabao mawili.

BERLIN

Bayern Munich imeendelea kuongoza kwa tofauti ya pointi 13 kwa Bayer Leverkusen katika Bundesliga baada ya kuichakaza Eintracht Frankfurt 5-0 Jumapili.

Mabao hayo matano yalifungwa na wachezaji tofauti wa Bayern: Mario Goetze, Franck Ribery, Arjen Robben, Dante na Mario Mandzukic.

Bayern imeweka rekodi ya kutokufungwa mechi 44, huku wakishinda mechi 17 kati ya 19 za ligi msimu huu, huku mechi mbili wakitoka sare. 


Chanzo: mwanaspoti
Previous Post Next Post

Popular Items

WAKUU WA USALAMA KUHOJIWA KENYA