Aliyekuwa meneja wa Chris Brown Amevujisha nyimbo za album mpya ya ‘X’ 'Chris Brown amshutumu'

Ikiwa ni siku moja toka msanii wa R n B Chris Brown atangaze tarehe ya kutoka kwa album yake ya ‘X’ ilioyoahirishwa mara kadhaa mwaka jana, ameibuka na kumshutumu meneja wake aliyepita kwa kuvujisha nyimbo za album hiyo.



Chris Brown ambaye pia amemaliza programu ya kukaa rehab siku tisini kama alivyoamuriwa na mahakama mwaka jana (2013), amesema licha ya aliyekuwa maneja wake kuvujisha nyimbo zake pia amekataa kumpatia ‘backup hard drive’ yake yenye nyimbo hizo ili aifanyie hujuma.
Breezy alitweet, ‘My old manager is leaking my NEW album music and refuses to give me my backup hard drive to sabotage my album.’



Hata hivyo baadaye Breezy aliifuta tweet hiyo.

Baada ya tweet ya mwimbaji wa ‘Fine China’, aliyekuwa meneja wake aitwaye Tina naye aliamua kumjibu kwa kuandika:

‘@chrisbrown Trace it! Find out where it originated from…RCA can do that for you. Then send a defaming tweet out on who really did it.’ Tweet ambayo pia ilifutwa baada ya muda.

Tina aliongeza tweet nyingine:
‘My career started 10 years before I met @chrisbrown. It grew another 10 years afterwards….#Godisgreat #Godgotme #Godgotus Thank you!!!!’

Album ya X ambayo iliyokuwa itoke July mwaka jana sasa imepangwa kutoka May 5 mwaka huu.
Previous Post Next Post