Kikosi cha Mapinduzi kilichopambana na kuleta Mapinduzi ya Zanzibar kikipita mbele ya jukwaa kuu na kutoa heshima kwa Rais wa Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein,kwenye kikosi hicho amebaki mwana mama mmoja anayefahamika kwa jina la Fatma Abdalla Mussa watatu kutoka kulia.
Vijana wa Halaiki wakionyesha ushiriki wao kwenye miaka 50 ya Mapinduzi "Mapinduzi Daima".
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia mamia ya wakazi wa Zanzibar wakati akiwasili kwenye Uwanja wa Amani kwenye kilele cha sikukuu ya miaka ya 50 ya Mapinduzi.
Sehemu ya Umati uliofurika wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Maandamano mbali mbali kutoka kwenye Mikoa na Taasisi za serikali na zisizo za Serikali yalipita mbele ya jukwaa kuu na kutoa heshima kwa Rais wa Zanzibar na viongozi wengine.
Wakina mama hawakuwa nyuma kwenye maandamano ya mika 50 ya Mapinduzi kwenye uwanja wa Amani Zanzibar.
Kikosi cha Mbwa kikiingia uwanjani tayari kuonyesha umati wa watu jinsi Mbwa wenye mafunzo wanavyoweza kufanya kazi zao vizuri.
Askari wakionyesha jinsi askari waliokuwa chini ya mkoloni walivyokuwa wanafanya mambo yao ikiwa kila amri kutoka kwa lugha ya kiingereza.
Kikosi cha Makomandoo wakionyesha namna ya kupambana na maadui bila kutumia silaha za moto kwenye uwanja wa Amani wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Kikosi cha Kifaru kinaonyesha kifaru cha kivita.