Misa ya shukurani yafanyika nchini kenya kwa ajili ya mafanikio aliyoyapaya Muigizaji Lupita Nyong’o

Kufuatia mafanikio makubwa aliyoyapata muigizaji Mkenya aliyefanikiwa sana na kumake headlines hivi sasa huko Hollywood na katika ulimwengu wa filamu, Lupita Nyong’o amefanyiwa misa ya shukurani jijini Nairobi kwa lengo la kumshukuru Mungu kwa mafanikio anayoendelea kuyapata star huyo mpya wa filamu.



Marafiki na familia ya Nyong’o ambaye ni Mkenya aliyezaliwa Mexico huku wazazi wake wote wakiwa ni Wakenya, wamemfanyia misa hiyo Jumapili iliyopita katika kanisa la Ridgeways Baptist.

Hii ilikuwa pia ni njia mojawapo ya kushehereka mafanikio yake ya Hollywood ambapo amefanikiwa kunyakua tuzo kadhaa kutokana na ushiriki wake mzuri katika filamu ya ‘12 Year A Slave’.

Mark Wahlberg Akiwa na Lupita Nyongo's


Lupita amekuwa akipata support pia ya baba yake mzazi Anyang Nyong’o ambaye ni Seneta wa Kisumu pamoja na mama yake.

Katika moja ya mahojiano aliyofanya na mtangazaji Jimmy Kimmel, Lupita amsema umaarufu alionao hivi sasa nchini Kenya unaweza kuzidi wa baba yake ambaye ni seneta.


Vipande vya Movie aliyoifanya Lupita ya 12 Years a Slave



Vipande vya Movie aliyoifanya Lupita ya 12 Years a Slave

Umaarufu wa Lupita umeanza si muda mrefu sana, ni baada ya filamu ya ’12 Years A Slave’ kutoka mwaka jana. Lupita ni Mjaluo ambaye anazungumza Kijaluo, Kiingereza, Kiswahili, Kiitaliano na Kihispania.

Tazama moja ya interview yake hapa chini


Source: Nairobi Wire
Previous Post Next Post