Makala: Kwanini Ali Kiba hawezi kuja Kushuka kimuziki...

Leo katika makala yetu tunamuongelea ali kiba au a.k.a Kiba 4 Real Mwanamuziki wa Bongoflavour na aliyeanza kusikika kitambo kidogo kabla ata ya Diamond kusikika. ali kiba ni msanii mwenye uwezo mzuli sana wa kuimba na naweza nikasema kwamba sauti yake ndio ile yakumtoa nyoka pangoni mwake, ni muda mrefu sasa ali kiba ajapata kuhit katika tasnia nzima ya muziki wa ongo Flavour lakini ni msanii amabaye atokuja kushuka kimuziki.

Ingekuwa ni msanii mwingine ungesikia ameshapotea katika ramani hii ya muziki kutokana na ukimya wake ila siyo Ali kiba,akiwa ndiye nominee wa tuzo za KORA 2012,mwaka jana ni mwaka ambao msani huyu aliweza kukaa kimya kwa muda mrefuhuku watu wengi wakihisi kuwa ameacha muziki kabisa,ila si hivyo,Kati ya wasanii wa hapa Bongo wanaoheshimika sana basi Ali Kiba anapewa nafasi ya kipekee kutokana n uwezo wake wa kuimba na kule kutokuwa na drama nyingi za hapa na pale kama kawaida ya wasanii wengi wa muziki huu wa Bongo hasa pale wanapopata umaarufu,kuongelea kuhusu Ali kiba unaweza kusema ni mfano wa msanii wa Bongo fleva,ni moja ya msanii ambaye nyimbo zake zimeweza kukaa muda mrefu bila kuisha ile ladha ya muziki wake.


Mbali na ukimya alionao wa mwaka mzima wa jana,ila bado hata wasanii wenzake wamekuwa wakimkubali sana,kutokana na uwezo mkubwa wa kuimba aliokuwa nao,kwa wasanii wanaochipukia,alikiba amekuwa kama reference point,yani wasanii wanangalia wafanye muziki ili wafike level kama zake Ali Kiba,ikiwa ni pamoja na kuwa na ndoto zakufanya kazi na msanii huyu.
Mwishoni mwa mwaka jana msanii chipukizi Naylee alifunguka na kusema kuwa nyimbo za Ali Kiba ndizo zilizomfanya aweze kupata moyo na kuingia katika maswala haya ya muziki na kuwa na ndoto siku moja kufanya kazi na Ali Kiba.huyu ni mmoja tu ya wasanii chipukizi mwenye ndoto za kufanya kazi,hivyo mbali na kuwa kimya kwa muda Ali kiba bado amekuwa kwenye ndoto ya kila msanii kutaka kufanya nae kazi.


Nyimbo za Ali Kiba,kutokana na wadau mbali mbali waishio nje ya nchi,wanasema kuwa hupigwa sana huko nje ya nchi,moja ya nchi zinazopiga sana nyimbo za ali kiba ni huko Muscat,Inasemekana ni msanii wa bongo fleva anayesikilizwa kuliko msanii yeyote yule,hata kwa wale wasiojua kiswahili wamekuwa wakisikiliza nyimbo zake,..unaweza kufananisha haya yote na nyimbo za michael jackson hivi leo,sidhani kama watu wengi wanaopenda nyimbo zake wanajua kingereza,ila bado wanasikiliza na kuzicheza.
Ukirudi hapa East Africa ali kiba bado anacheza role kubwa kwenye list ya kila mmoja ya nyimbo azipendazo,na huko nchini kenya mbali na kutotoa hit single kwa kipindi cha muda mrefu,ni moja ya msanii anayeongoza kwa nyimbo zake kuwa requested sana,hii yote inaonyesha kuwa bado nyimbo zake zinapendwa sana na watu,haijalishi nyimbo ni ya mwaka gani.


Ni moja ya msanii aliyekuwa poa sana kusaidia wasanii wadogo wanaochipukia na hivyo kuwa kioo cha msanii ambaye anajali sana na kuheshimu kazi za mtu mwingine,ukiongelea ali kiba ni msanii ambaye yuko social sana na ameweza kusaidia wasani wengi sana wanaochipukia kimawazo na hata kufanya nao collabo katika nyimbo zao,imekuwa kawaida sana kwa wasanii wakubwa baada ya kupata umaarufu kusahau walipotoka kuwa wao pia mwanzo walikuwa chipukizi wakitafuta njia yakutokea kwa kukataa kabisa kufanya collabo na wasanii wachanga,but kwa Ali kiba ni tofauti kabisa,mbali na umaarufu wake mkubwa amekuwa msaada mkubwa kwa wasanii wanaochipukia,Talking about Ali Kiba ni moja ya msanii mkubwa wakuigwa.

Previous Post Next Post

Popular Items