Eve avishwa pete ya uchumba na Mbunifu wa mitindo wa Uingereza

Rapper mkongwe wa kike kutoka Marekani Eve Jihan Jeffers ‘EVE’ amethibitisha kuwa amechumbiwa rasmi, na hivi karibuni anatarajia kufunga ndoa na mpenzi wake ambaye ni mbunifu wa mitindo wa Uingereza Maximillion Cooper.


Eve na Cooper wamekuwa wapenzi kwa takribani miaka mitatu sasa.


Cooper alimwomba uchumba EVE mwenye miaka 35 siku ya Christmas ya mwaka jana 2013 huko Edinburgh, Scotland walipoenda kusheherekea sikukuu.


Kama wafanyavyo wasichana wengine wanapoingia katika status ya ‘uchumba’, EVE aliionesha pete yake ya uchumba ya almasi kupitia Instagram na kuandika,
“Asante kwa kila mmoja kwa pongezi zenu za engagement! Tulitaka kusheherekea na familia yetu na marafiki kwanza kabla ya kutangaza”.

Eve akiwa na mama yake na kaka yake, tayari pete ya uchumba ikiwa kidoleni

Baadaye mchumba wake naye aliandika kupitia ukurasa wake “Yes it’s official…I asked the question…and she said YES! WAHOOO! we’re getting married!”.

Hii itakuwa ni ndoa ya kwanza kwa Eve, wakati mume wake mtarajiwa tayari ana watoto wanne waliopatikana katika ndoa zake zilizopita.
Previous Post Next Post

Popular Items