Baba wa mwanasoka Neymar ametetea suala la malipo ya kabla ya €10 million ambayo Barcelona ililiipa kampuni yake miaka mitatu iliyopita ili kupata upendeleo katika kugombea saini ya mchezaji huyo.
Barcelona waliizidi nguvu Real Madrid katika kuwania saini ya mshambuliaji huyo, mwenye miaka 21 ambaye wiki iliyopita uhamisho wake ulileta matatizo Nou camp, na kumfanya Sandro Rosell kujiuzulu kuwa Raisi wa klabu hiyo baada ya kufunguliwa kwa kesi ya matumizi mabaya ya fedha katika usajili wa Neymar.
Jana Jumanne, Neymar Sr alikiri Barca walimpa €10m mwaka 2011. Hii ilikuwa ni sehemu ya malipo ya €40m waliyomlipa kwa ujumla kuhakikisha Barca wanapewa nafasi ya kwanza katika uhamisho wowote wa Neymar, lakini akasisitiza kwamba hawakuvunja sheri a kwa makubaliano hayo binafsi na ya siri. Fedha hizo ilizolipwa kampuni ya baba yake Neymar zingerudishwa endapo mchezaji huyo asingejiunga na klabu hiyo, alisema baba mzazi wa Neymar.
“Barcelona walinilipa €10m [mnamo 2011],” Neymar Sr aliiambia ESPN Brasil, baada ya kufanya mkutano na waandishi wa habari nchini Brazil.
“Sio kosa la kisheria. Barca hawakumlipa Neymar, waliilipa kampuni yangu (N&N, inamilikiwa na wazazi wa Neymar].
“Nini nilifanyia zile €10m? niliziweka kwenye bima ili ikitokea chochote kwa Neymar, ikiwa angepata majeruhi, kwa mfano, bass ningeweza kulipa deni la €40m.”
Tags:
Sports