ARSENAL YAREJEA KILELENI, MAN U WABWAGWA

HALI mbaya kwa kocha David Moyes, baada ya juzi Manchester United kuuanza mwaka vibaya kwa kipigo cha mabao 2-1 nyumbani kutoka kwa Tottenham Hotspur katika mchezo wa Ligi Kuu ya England, Uwanja wa Old Trafford.


Mabao ya yaliyoizamisha United nyumbani jana yalifungwa na Adebayor dakika ya 34 na Eriksen dakika ya 66, wakati bao pekee la Mashetani Wekundu lilifungwa na Welbeck dakika ya 67.

Matokeo hayo yanazidi kuondoa matumaini ya United kutetea ubingwa msimu huu, ikiwa inabaki na pointi zake 34 baada ya kucheza mechi 20 na kushuka hadi nafasi ya saba, wakati Spurs sasa inasogea nafasi ya sita kwa kufikisha pointi 37, baada ya kucheza mechi 20 pia.

Katika mchezo mwingine wa ligi hiyo, Liverpool imaibwaga Hull City mabao 2-0, wafungaji Agger dakika ya 36 na Suarez dakika ya 50.
Chelsea imeifunga Southampton 3-0, mabao ya Torres dakika ya 60, Willian dakika ya 71 na Oscar dakika ya 82.
Arsenal imeichapa Cardiff 2-0, mabao ya Bendtner dakika ya 88 na Walcott dakika ya pili ya muda wa nyongeza baada ya kutimu dakika 90 za kawaida za mchezo.

Crystal Palace imetoka 1 - 1 na Norwich City, Fulham imeifunga 2 - 1 West Ham United, Stoke City imetoka 1 - 1 na Everton, Sunderland imefungwa 1-0 nyumbani na Aston Villa na West Bromwich imeilaza 1 - 0 Newcastle United.
Arsenal inaendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi zake 45 baada ya kucheza mechi 20, Manchester City iliyoifunga 3-2 Swansea City ya pili kwa pointi zake 44, Chelsea ya tatu pointi 43 na Liverpool ya nne pointi 39, wakati Everton yenye pointi 38 ni ya tano.
Previous Post Next Post