2Face Idibia Apata Mtoto Mwingine Wa Kike

Msanii aliyehit na wimbo wa my african queen na mwenye mafanikio makubwa nchini Nigeria, 2Face Idibia na mkewe Annie Idibia ambaye ni mwigizaji wa Nollywood wamefanikiwa kupata mtoto mwingine wa kike baada ya Annie kujifungua salama siku ya Jumamosi jijini Atlanta Georgia Marekani.


Wapendanao hawa wawili tayari wameshafanikiwa kupata mtoto wa kwanza awali ambaye atakuwa na umri wa miaka mitano kwa sasa waliyembatiza jina la Isabella, kwa sasa familia ya msanii 2face imapanuk baada ya kubahatika kupata mtoto mwingine wa pili
Annie Idibia Akiwa na Mtoto wake mara Baada ya Kujifungua
Previous Post Next Post