Wastara amuandikia ujumbe wa kumkumbuka mumewe Sajuki ambaye mwezi ujao atatimiza mwaka mmoja tangu afariki dunia 'Instagram'

Mwezi ujao (January 2) aliyekuwa muigizaji wa Bongo Movie marehemu Juma Kilowoko maarufu kama Sajuki atafikisha mwaka mmoja tangu afariki dunia. Mkewe Wastara Mohamed (Wastara Sajuki) ameandika ujumbe wa kumkumbuka kipenzi chake kupitia Instagram.


“Siku week mwezi hatimae mwaka unaingia tokea ukimbie mikononi mwangu mwetu, milele nitakukmbuka daima nahisi uko sehemu nzuri unanisubiri, tal 2/1/2014 my bld anatimiza mwaka tokea atutoke katika hii dunia, nawaomba tuwe pamoja katika duwa itakayofanyika mkoani songea kokte ulipo inua mikono kumuombea juma kilowoko aka sajuki and mboni ya wastara”. Ameandika Wasrata
Previous Post Next Post