USA: Eminem aomba alipwe shilingi ‘bilioni 3.2’ kwenye show ya Super Bowl

Eminem si rapper wa bei cheee. Rapper huyo anadaiwa kuomba alipwe si chini ya dola milioni 2 (zaidi ya shilingi bilioni 3.2) kutumbuiza kwenye Super Bowl.



Fainali za ligi ya NFL aka The Super Bowl ni maarufu kwa kushirikisha mastaa wakubwa kutumbuiza ‘half-time’ ambapo wasanii waliowahi kutumbuiza ni pamoja Madonna, The Who, Prince na Beyonce. Eminem aliombwa kutumbuiza kwenye ‘NFL Owners Party’ wakati wa wiki ya Super Bowl mwakani.

Alikuwa aende kutumbuiza nyimbo zake kali mbele ya wageni 1,500 lakini waandaji wakabidi watafute mtu mwingine kuchukua nafasi yake. Waandaji pia walikuwa wamepanga kumtafuta Kanye West lakini naye alidai kulipwa mkwanja mrefu, dola milioni 1 na masharti kibao.

Hata hivyo waandaaji walikuja kumpata msanii wa ‘Tight Rope’, Janelle Monae ambaye atatumbuiza kwa $150,000.
Previous Post Next Post