Tuzo ya mchezaji bora Africa Inayotolewa na BBC - 2013 Yachukuliwa na Yaya Ture Kutoka Ivory Coast

Kiungo wa klabu ya Manchester City ya Uingereza na Ivory Coast Yaya Toure ametangazwa mshindi wa tuzo ya BBC ya mwaka 2013 ya mchezaji bora zaidi wa soka barani Afrika.


Toure ambaye jina lake limekuwepo kwa miaka minne iliyopita katika orodha ya wachezaji wanaowania tuzo, aliwashinda Pierre-Emerick Aubameyang, Victor Moses, John Mikel Obi na Jonathan Pitroipa, katika kuibuka mshindi.


Orodha ya wachezaji waliowania tuzo hiyo ilitayarishwa na wataalamu 44 wa soka kutoka kote barani Afrika, na wakizingatia hasa maarifa ya mchezaji, kiufundi, ushirikiano na wenzake katika timu, na kwa kucheza mchezo safi na kwa haki na kisha, kupitia idadi kubwa kabisa kuandikishwa kwa wapiga kura, mashabiki waliweza kushiriki katika shughuli hiyo katika mtandao, au kupitia ujumbe wa simu ya mkononi.

Mashabiki hao wameamua kwamba Toure ndiye bora zaidi, kwani katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, raia huyo wa Ivory Coast alicheza kwa bidii, kuonyesha mchezo wa kasi, ubunifu, na vile vile kwa kufunga magoli.

Source:BBC
Previous Post Next Post

Popular Items