Ryan Seacrest awekeza tshs bil 1.6 kutengeneza iPhone yenye uwezo wa kuwa Blackberry

Ryan Seacrest Anayepatikana katika  kampuni ya utengenezaji vipindi vya reality TV, Ryan Seacrest Productions ambayo huandaa vipindi kama Kourtney & Kim Take New York na Kourtney & Kim Take Miami — anajua kutumia fursa kila aionapo.



Wakati ambapo simu za BlackBerry zinaendelea kupoteza kabisa umaarufu, mtangazaji huyo wa American Top 40 na host wa American Idol amejiuliza swali muhimu. Vipi kama ukichanganya umbo la nje keyboard ya BlackBerry na software ya simu ya iPhone?


Baada ya miaka miwili ya utengenezaji na kuweka dola milioni 1, sawa na shilingi bilioni 1.6, matokeo yake ni: The Typo iPhone Keyboard ambayo inaigeuza simu ya iPhone na kuwa BlackBerry. Keyboard hizo zitaanza kuuzwa January mwakani.







Sababu ya Seacrest kuanzisha simu za aina hiyo ni kwasababu alikuwa akiwaona marafiki zake wakibeba simu mbili. Moja kwaajili ya kutype haraka haraka na iPhone kwaajili ya kuona kila kitu katika mfumo wa kushika. Siku moja Ryan na rafiki yake Laurence Hallier, CEO wa Show Media, walikuwa wakipata dinner na wote walikuwa na simu mezani. Watu wawili, simu nne.

Keyboard hiyo itaifanya iPhone iwe na muonekano wa Blackberry lakini mfumo wa ndani wa simu ukiendelea kuwa ule ule wa iPhone.






Previous Post Next Post