Picha: Yaliyojiri Katika Mazishi ya Nelson Mandela

Mazishi ya Nelson Mandela Yamehudhuriwa na watu zaidi ya 7,000 kutoka katika nchi Tofauti Duniani, Nelson Mandela Jumapili hii amezikwa kijijini kwake alikozaliwa, Qunu katika jimbo la Eastern Cape nchini Afika Kusini .

Hata hivyo ratiba ya mazishi hayo ilizidisha muda kwa karibu masaa mawili na hivyo mila za kikabila kuwa mazishi yanatakiwa mchana wakati jua likiwa utosini ilibadilika.

Mandela alifariki December 5 akiwa na umri wa miaka 95.

Jeneza la Mandela likiwa limezungukwa na maafisa wa juu wa jeshi



Helikopta za kijeshi zilizokuwa zimebeba bendera za Afrika Kusini zilipita juu ya kaburi ikifuatiwa na saluti ya risasi 21

Wageni waliohudhuria ni pamoja na Rais Jakaya Kikwete na marais wengine wa Afrika, Prince Charles, Oprah Winfrey, Richard Branson mwanaharakati wa Marekani, Jesse Jackson.

Huyu ni Mjukuu wa Mandela, Nand akiongea mbele ya waombolezaji huko Qunu

Mke wa zamani wa Mandela Winnie (kushoto) Rais Jacob Zuma na mjane wa Mandela Graca Machel


Oprah Winfrey (katikati) akiwa na mume wake Stedman Graham (kushoto) na bilionea wa Uingereza Richard Branson

Prince Charles akisalimiana na wageni wengine



Ukumbi huu maalum ulijengwa kwa ajili ya kufanya maombi kabla ya mazishi ya Mandela

Wanajeshi hawa walisindikiza jeneza la Mandela hadi katika ukumbi maalum ambako ibada ya kumuaga Mandela ilifanyika

Waliokuwa wake za Mandela walikesha usiku kucha kabla mazishi kufanyika leo

Ngozi iliyofunikwa jeneza la Mandela kama ishara ya umuhimu wa Mandela katika jamii ya watu wa Thembu


Kuambatana na tamaduni za watu wa Thembu ukoo wa Mandela, jeneza la mfu hufunikwa kwa ngozi ya Ng'ombe ishara ya umuhimu wake katika jamii




Wakazi wa Qunu wakishuhudia kwa mbali mazishi

Previous Post Next Post