Picha: Samsung yazindua TV kubwa zaidi duniani, ina inch 102 na inapatikana kwa bei ya milioni 240

Kampuni ya Kikorea Samsung imeingiza sokoni TV mpya yenye upana wa inch 102 na urefu wa inch 70, ukubwa ambao ni zaidi na kitanda kikubwa (king-sized bed).


TV mpya ya Samsung iliyoingia sokoni jana

TV hiyo imeingizwa sokoni kwa mara ya kwanza Korea Kusini ikiwa inauzwa 160million won ya Korea Kusini sawa na shilingi milioni 241 za Tanzania.

TV hiyo inatumia teknolojia ya U-HDTV (Ultra-High Definition Television) inayosababisha picha kuonekana vizuri zaidi ya mara nne ya TV za HD za kawaida.


Toleo hili jipya la TV ya Samsung limechukua nafasi ya toleo lililopita la TV iliyokuwa kubwa zaidi kwa kampuni hiyo kuwahi kutengeneza ambayo ni inch 85.

TV mpya ya Samsung imeanza kuuzwa jana (Dec 30) Korea Kusini, lakini baadaye itaanza kupatikana sehemu mbalimbali duniani.
Previous Post Next Post

Popular Items

WAKUU WA USALAMA KUHOJIWA KENYA