Kama kijana, Mandela alipenda masumbwi. ''Masumbwi ni bure, Ukiwa ulingoni , umri na hadhi yako pamoja na mali yako sio muhumu,'' aliandika katika kitabu chake kuhusu maisha yake
Kampeini ya kimataifa ilianza dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi. Licha ya Afrika Kusini kuwekewa vikwazo vya kiuchumi, ingawa havikuwa vikali, wasanii mashuhuri na wananchi wa kawaida kote duniani waliendelea kushinikiza.
Mashauriano makubwa yalifanyika kabla ya rais FW de Klerk kukubali au kuruhusu watu kupiga kura. Wawili hao walituzwa tuzo ya amani ya Nobbel, kwa sababu ya kumaliza ubaguzi wa rangi Afrika Kusini.
Mandela alitawala nchi hiyo kwa muhula mmoja pekee na mnamo mwaka 1999 akawa mmoja wa viongiozi wachache wa Afrika kuachia ngazi kwa hiari. Thabo Mbeki, alipewa jukumu la kumrithi Mandela kama rais na kiongozi wa ANC
Kando na kuwa kiongozi anayependwa zaidi duniani, pia aliweza kuonekana na mitindo ya kipekee kwa sababu ya T sheti zake nzuri nzuri. Hapa anawaluiza wandishi wa habari maoni yao kuhusu shati yake, baada ya maankuli ya mchana na muundajji wa mitindo Pierre Cardin
Pia ana mambo mawili ambayo sio kawaida kwa viongozi wa dunia kuwa nayo....mpole na mwenye kuweza hata kujicheka , hapa anakutana na mwanamfalme Prince Charles na wanamuziki wa iliyokuwa bendi ya Spice Girls
Baada ya kutalakiana na mkewe Winnie , Mandela alimuoa Graca Machel, alipokuwa anasherehekea miaka 100m mwaka 1998. Bi Machel ni mjane wa aliyekuwa rais wa Msumbiji Samora Machel. Bi Graca na Mandela walianzisha hazina ya kuwasaidia watoto wasio na uwezo mkubwa maishani
Bwana Mandela, aliweza kujitokeza wakati wa sherehe ya kufunga michuano ya kombe la dunia mwaka huo. Hali yake ya kiafya ilikuwa mbaya na alikuwa anaomboleza kifo cha kitukuu wake aliyeuawa huku michuano hiyo ikianza.
R.I.P NELSON MANDELA
Image Credit:BBC