Joh Makini na Nikki wa Pili kufanya video tatu mwezi January 2014

Rappers ndugu wa kampuni ya Weusi Joh Makini na Nikki wa Pili, mwezi January 2014 wanatarajia kufanya video tatu za nyimbo zao zilizotoka na hazina video mpaka sasa.




Joh amesema kuwa video ya kwanza wanatarajia kuifanyia jijini Arusha wiki hii na director Nisher, na kuwa wanatarajia kuondoka kesho (Dec 31) pamoja na G-Nako kuelekea Arusha kwaajili ya kazi hiyo.

Amesema video ya pili ambayo itakuwa ya single yake na Nikki wa Pili ‘Bei ya Mkaa’ itafanyika Dar es salaam chini ya muongozaji Adam Juma, katika wiki ya pili au ya tatu ya January.

Makini ameongeza kuwa video ya tatu anayotegemea kuifanya mwezi January mwakani ni ya single yake ‘Nikumbatie’ ambayo audio ilitengenezwa na Fundi Samweli. Joh amesema video ya wimbo huo anategemea kuifanya na director wa nje.

“Sijajua nafanya na nani video ya Nikumbatie lakini nataka kufanya na director wa nje…naweza kuja au mimi kwenda ila nitajua nikishaamua ni nani nafanya nae” Alisema mwamba wa Kaskazini.
Previous Post Next Post