Album Mpya ya Beyonce Aliyoiachia Hivi karibuni Yavunja Rekodi kwa Kununuliwa Mara Nyingi zaidi

Album mpya ya Beyonce, yenye jina lake na iliyotoka kwa kushtukiza inaelekea kukamata nafasi ya kwanza kwenye chart ya Billboard 200 wiki hii.





Unaambiwa Tayari Album ya Beyonce inayouzwa kupitia mtandao wa iTunes imeshanunulia kwa zaidi ya 550,000 nchini Marekani tangu Jumamosi usiku. Santuri hiyo inaweza kuuza hadi kopi 600,000 hadi kufikia leo asubuhi.

Album hiyo yenye nyimbo 14 na video 17 inauzwa kwa $15.99.

“Beyonce” tayari ni album iliyouza zaidi katika wiki ya kwanza kwa msanii wa kike tangu ile Taylor Swift, Red iliyouza kopi milioni 1.2.
Previous Post Next Post