ZITTO KABWE : “NILISHIKWA BUTWAA, WAKATI HUO WATU WENGI WALIMDHARAU MBUNGE HUYU….”

Hivi ndivyo mbunge kutoka Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe alivyoelezea uhusiano wake wa kazi na Marehemu Amina Chifupa.
“Kazi ya kwanza nilifanya Bungeni ilikuwa ni kuhesabu kura za kumthibitisha Waziri Mkuu Edward Ngoyai Lowasa. Spika Samwel Sitta aliteua mbunge mwenye umri mdogo zaidi na mbunge wa kuchaguliwa mwenye umri zaidi.




Amina Chifupa na mie tulienda kuhesabu kura zile. Kura 3 ziliharibika. Karani wa Bunge akatuomba tusirekodi kura zilizoharibika kwani ni aibu kwa wabunge.

Amina akakataa kwa kusema “aibu gani, wananchi wawajue wabunge wao”! Nilishikwa butwaa.

Wakati huo watu wengi walimdharau mbunge huyu kama ‘mtangazaji’ tu tena wa mipasho. Jioni ya siku ile Disemba 29, 2005 ilibadili kabisa mtazamo wangu kuhusu watu na uwezo wao. Amina alishangaza wengi kiuwezo hasa vita yake dhidi ya dawa za kulevya.”
Previous Post Next Post