UFARANSA YAIFUNGA UKRAINE 3-0 NA KUFUZU KOMBE LA DUNIA.

Ufaransa imefanikiwa kufuzu kucheza Kombe la Dunia baada ya kuigeuzia kibao Ukraine na kuichapa mabao 3-0. Awali Ukraine ilishinda kwa mabao 2-0 ikiwa nyumbani na kuweka matumaini ya juu kusonga mbele katika mechi hiyo ya marudiano ugenini. 


Lakini leo kwa mabao ya Mamadou Sakho aliyefunga mawili na Karim Benzema, Ufaransa imetinga fainali ya Kombe la Dunia. Ilionekana ni vigumu kwa Wafaransa kusonga mbele baada ya kufungwa mabao 2-0 katika mechi ya kwanza.

Previous Post Next Post