PICHA: MTAZAME RAY C AKIFURUHI NA WAATHIRIKA WA DAWA ZA KULEVYA UKZINGATIA NI MWAK 1 TANGU AACHE KUZITUMIA

Rehema Chalamila aka Ray C amesherehekea na vijana waliokuwa wameathirika wa dawa za kulevya, kuadhimisha mwaka mmoja tangu aachane na matumizi ya dawa hizo.


Kupitia Instagram Ray C amepost picha akiwa na waathirika hao ambao nao wameachana na matumizi ya madawa ya kulevya.


“8/11/2013 ni Siku muhimu sana kwangu Asante Mh Rais Jakaya Kikwete…..Milele Ubarikiwe kwa kunisaidia kunileta kitengo Hiki na kutuletea watanzania hii dawa ya Methadone Tanzania…….We Love You,” ameandika.

“Nawapenda sana hawa wenzangu wote tuligundua tatizo tukasaidiwa na sasa tumepona na tunamshukuru Mungu….Tanzania bila Madawa ya Kulevya inawezekana. Hujui lini yatakutokea mami usihukumu wala kudharau Mtu katika Maisha yako kwani wewe huna mkataba na Mungu wala hii dunia si yako omba sana usije pata mtihani Mgumu Zaidi ya Sisi wenzako� Aliandika Ray C.


Previous Post Next Post