Kundi zima la P Square limeshawasili jijini Dar es salaam TAayari kwa Shoo yao inayowakabili leo pale Leaders Club,P square waliwasili nchini usiku wa juzi ambapo jana walipata muda wa kuweza kuongea na waandishi wa vyombo vya habari na kufanya shughuli za kijamii, pata muda wa kuzitazama picha hizi za P Square wakiwa katika shughuli hizo za kijamii jijini Dar es salaam.
Paul Okoye wa kwanza kulia, akizungumza na waandishi wa habari (hawako pichani) kuhusu tamasha watakalolifanya kesho Jumamosi. Novemba 23 katika viwanja vya Leaders Club, jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Peter Okoye ambao kwa pamoja wanaunda kundi la P Square, wakiwa na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twisa ambao ni wadhamini wa wasanii hao pamoja na Lady Jay Dee mmoja wa wasanii watakaowasindikiza jukwaani wasanii hao.
Mkuu wa Kitengo cha Vodacom Foundation, Yesaya Mwakifulefule akipeana mkono na wasanii, Peter na Paul Okoye, maarufu kama P Square wakati walipowasili kwenda kutoa msaada katika kituo cha watoto wenye ulemavu wa usonji “Autism” (utindio wa ubongo) cha Msimbazi Mseto, jijini Dar es Salaam.
Peter Okoye akimuweka vizuri katika bembea mmoja wa wanafunzi wenye ulemavu wa usonji katika shule ya Msimbazi Mseto jijini Dar es Salaam. Wa kwa nza kutoka kushoto ni mwalimu Mkuu wa shule hiyo Reuben Gadi na Mjumbe wa bodi ya shule hiyo Mtumwa Nindi, na wa kwanza kulia ni mfanyakazi wa Vodacom Tanzania Precious Hughes ambao ni wadhamini waliofanikisha wasanii hao kutua nchini.
P Square (Peter na Paul Okoye) katikati wakimsikiliza Mtoto mwenye ulemavu wa Usonji, Erick wa shule ya msimbazi Mseto walipokwenda kushiriki kutoa msaada kwa kituo cha watoto hao. Wa kwanza kushoto ni mwalimu mkuu wa shule hiyo Reuben Gadi na kulia ni Mkuu wa kitengo cha Vodacom Foundation, Yesaya Mwakifulefule pamoja na wafanyakazi wengine wa kampuni hiyo.
P Square wakikabidhi misaada mbalimbali kwa watoto wenye ulemavu wa usonji wa kituo cha Msimbazi Mseto cha jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa kitengo cha Vodacom Foundation, Yesaya Mwakifulefule akishuhudia makabidhiano hayo, na katikati ni walimu wa shule hiyo wakipokea kwa pamoja misaada hiyo.
Image Cerdit via:Vodacom