NISHER KUANZA KUTOZA MILL 6 KWA KILA VIDEO

Muongozaji wa video nchini, Nisher, anatarajia kuwa muongozaji wa video za muziki anayetoza fedha nyingi zaidi nchini.


Nisher amesema kwa sasa anatoza shilingi milioni 3 kwa video moja lakini pindi vifaa vyake vipya na vya kisasa vitakapowasili, ataanza kutoza dola 4,000 kwa video moja ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 6.

“Sitaki kufanya kazi na kila mtu eti kwasababu mimi ni director,” amesema Nisher. “Nataka niwe na heshima yangu fulani yaani mtu akifanya kazi na mimi ajisikie kwa proud kuwa kitakachotoka sio cha mchezo. So kwangu bora mtu alipe ghali akiwa uhakika wa kazi kuliko amlipe tu director yeyote bei rahisi halafu kazi mbaya.”

Video alizowahi kuziongoza Nisher ni pamoja na Jikubali ya Ben Pol, Amani ya Moyo ya Feza Kessy, Kijukuu ya Young D, 2030 ya Roma, Nakomaa na Jiji ya Shilole, Sumu ya Lucci, Baby ya Mirror, Bila Wewe ya Jordan ft Mirror na Ngwea na zingine.
Previous Post Next Post