NEY WA MITEGO ADAI MUZIKI UMEMUINGIZIA ZAIDI YA TSH MILL 80 KWA MWAKA HUU

Rapper Nay wa mitego amefunguka kwa kusema kuwa ndani ya mwaka huu ameingiza zaidi ya shilingi milioni 80 kutokana na muziki pamoja na baadhi ya matangazo madogo madogo aliyoyafanya.


Nay alisema tangu ameanza kufanya muziki hajawahi kufulia.

“Kama kujenga nilishajenga tangu hata sijaanza kufanya muziki,na sasa hivi nimekuwa nikijitaidi kufanya muziki wangu kama ndio mtaji wa maisha yangu ndio maana hata kuna baadhi ya deal za matangazo nimekuwa nikizikataa kutokana na bei.Kama mtakumbuka nilhitajika niwe judge katika mashindano ya BSS lakini nilishindwa nao kutokana niliona haina maslahi kwangu,” alisema Nay.

“Kuna kampuni ya simu ilinipigia simu kunihitaji mimi niwe balozi na kufanya baadhi ya matangazo ila bado hatujafika muafaka ,tupo kwenye makubaliano ya bei.Kama ningekuwa msanii njaa ungenikuta kwenye matangazo,lakini nahitaji kama tukikubaliana na mimi ninufaike vizuri.”

Previous Post Next Post

Popular Items