MATAJIRI 50 WA AFRICA : KUTOKA TANZANIA NI WANNE NA ROSTAM AZIZ NDIYE BILIONEA PEKEE TZ

It’s official, Rostam Aziz ndiye bilionea pekee wa Tanzania (kwa dola). Kwenye orodha mpya ya matajiri 50 wa Afrika, Rostam Aziz ameingia kwa mara ya kwanza na kwa kishindo.


Utajiri wake umechangiwa zaidi na kuwa na asilimia 35 ya hisa za kampuni ya Vodacom Tanzania, yenye watumiaji zaidi ya milioni 9.5. Anamiliki kampuni ya Caspian Mining, inayotoa huduma za uchimbaji kwenye migodi mikubwa nchini inayomilikiwa BHP Billiton na Barrick Gold. Utajiri wake unamfanya awe mtu wa pili Afrika Mashariki kuwa bilionea nyuma ya Sudhir Ruparelia wa Uganda na pia kukamata nafasi ya 27 kwenye orodha ya Forbes mwaka huu.

Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP, Reginald Mengi amemfuata kwa mbali Rostam kwa kuwa na utajiri wa dola milioni 550 na kukamata nafasi ya 34 kwenye orodha hiyo ya Forbes.


Utajiri wa Mengi, ambaye naye ndio ameingia kwa mara ya kwanza kwenye orodha ya matajiri wa Afrika umetokana na kuwa na himaya kubwa ya vyombo vya habari. Anamiliki magazeti 11 yakiwemo Nipashe, Financial Times, ThisDay na The Guardian, vituo vya TV, (EATV, Capital na ITV), Radio One, EA Radio na Capital FM. Mengi pia anamiliki mgodi wa dhahabu pamoja na kiwanda Coca-Cola.

Kwenye nafasi ya 38 wapo Said Salim Bakhresa na Mohammed Dewji wenye utajiri wa dola milioni 500 kila mmoja.


Kwenye orodha hiyo, tajiri wa Nigeria Aliko Dangote anayemiliki kiwanda cha saruji mjini Mtwara ameendelea kukamata namba moja kwa kuwa na utajiri wa zaidi ya dola bilioni 20.

Ingia hapa kuona orodha nzima ya Africa’s 50 Richest.
Previous Post Next Post