Msanii Linex Sunday Mjeda aka The V.O.A ameamua kufungua ukurasa wa pili wa kipaji ambacho hajawahi kukionesha cha uigizaji, hivi karibuni ataonekana katika filamu mpya ya muigizaji wa bongo movie Aunty Ezekiel inayoitwa ‘MWAJUMA’.
“Movie inaitwa Mwajuma, Mwajuma alikuwa mama ntilie tu wa mgodini maisha yakamnyookea akawa anabadilisha wanaume kama nguo.” Alisema Linex
Katika movie hiyo ambayo ndiyo ya kwanza kwa msanii huyo wa ‘Kimugina’, Linex amecheza kama mmoja wa wanaume waliopangwa foleni na Mwajuma, “So mimi ni ni mmoja wa wanaume wa Mwajuma niliyebadilishwa kama nguo”. Alisema Linex