KAMPUNI YA AAPLE NA SUMSUNG WAPELEKEANA TENA MAHAKAMANI

Apple na Samsung wanarudi tena mahakamani kwenye kesi yao maarufu ya haki miliki. August 2012, jopo la waamuzi wa mahakama liliikuta Samsung na hatia kwa kuiba ‘vitu’ (patent) sita vya Apple na kulipwa kiasi kikubwa cha fedha.

Hukumu hiyo na faini ya dola bilioni 1 ilionekana kama ushindi kwa Apple. Hiyo ni moja tu ya kesi nyingi za haki miliki makampuni hayo yanagombana kwenye mahakama duniani kote. March 2013, jaji alipitia kiwango hicho cha dola bilioni 1 na kupunguza kiasi hicho na kusema hasara hiyo itafanyiwa tathmini kwenye kesi mpya.

Jaji Lucy Koh alisema jopo la waamuzi wa mahakama ya California lilipiga hesabu vibaya sehemu ya hasara hiyo. Alisema kiasi cha dola milioni 550 zimeshafanyiwa kazi lakini dola milioni 450 zilizosalia zitaangaliwa tena.

Awali Apple ilitaka ilipwe dola bilioni 2.5 kutoka kwa Samsung.

Previous Post Next Post

Popular Items